Jumatano 11 Novemba 2026 - 13:08
Maadhimisho ya Tamasha la Utamaduni la Bibi Fatimah Zahraa (s.a.) Yafanyika Katika Chuo Kikuu cha Baghdad kwa Ushiriki wa Wanafunzi 1,500 + Picha

Hawza/ Atabat Abbasiyya Tukufu imeandaa Tamasha la 11 la Utamaduni la kila mwaka la Bibi Fatimah Zahraa, maarufu kwa jina la As-Siddiqah At-Tahirah (s.a.), katika Chuo Kikuu cha Baghdad nchini Iraq. Tamasha hilo limeandaliwa na Idara ya Mahusiano ya Umma ya Atabat Abbasiyya, ndani ya mradi wa kitaifa wa Fityatu Al-Kafeel, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Baghdad.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ataba Abbasiyya Tukufu imefanya Tamasha la 11 la Utamaduni la kila mwaka la Bibi Fatimah Zahraa, maarufu kwa jina la As-Siddiqah At-Tahirah (s.a.), katika Chuo Kikuu cha Baghdad.

Sayyid Ahmad Al-Yasiri, ambaye ni msimamizi wa Kitengo cha Mahusiano ya Vyuo Vikuu katika Ataba Abbasiyya, alisema kuwa tamasha hilo lilianza kwa kupigwa na kuimbwa wimbo wa taifa wa Iraq, kisha ikasomwa Suratul-Fatiha.

Maadhimisho ya Tamasha la Utamaduni la Bibi Fatimah Zahraa (s.a.) Yafanyika Katika Chuo Kikuu cha Baghdad kwa Ushiriki wa Wanafunzi 1,500 + Picha

Baada ya hapo, kulikuwa na usomaji mzuri wa baadhi ya aya za Qur'ani Tukufu kwa sauti ya msomaji wa Qur'ani, Sayyid Hussein Al-Askari.

Aidha, hotuba kwa niaba ya Ataba Abbasiyya ilitolewa na Dkt. Hassan Dakhil, na kufuatiwa na hotuba ya Rais wa Chuo Kikuu cha Baghdad, Dkt. Alaa Abdulhassan Al-Zughaybi.

Vilevile, katika mwendelezo wa shughuli za tamasha hilo, Sheikh Mitham Al-Khafaji alitoa mhadhara wa kitamaduni, huku washairi Muhammad Al-Fatimi na Muhammad Al-Yasiri wakitoa mashairi yao.

Aliongeza kuwa katika tamasha hilo, wanafunzi wa kike 1,500 walitunukiwa zawadi na kutambuliwa kwa lengo la kuwahamasisha kuvaa vazi la Abaya ya Kiiraqi wanapokuwa katika maeneo ya chuo kikuu. Tamasha hilo lilipokelewa kwa hamasa kubwa na kushirikishwa kwa upana na wanafunzi wa kike.

Ataba Abbasiyya Tukufu inaweka mkazo katika kupanua uwepo na shughuli zake ndani ya vyuo vikuu nchini Iraq kupitia miradi na programu mbalimbali zinazolenga kuimarisha utambulisho wa kidini na kitaifa miongoni mwa vijana, pamoja na kuimarisha tunu za kimaadili katika jamii za vyuo vikuu.

Vilevile, Ataba Abbasiyya inaunga mkono wanawake wanaopata elimu ya juu na kuwahimiza kushikamana na utambulisho wao halisi. Hatua hiyo inalenga kuwasaidia wanawake hao kushiriki katika malezi ya kizazi chenye uelewa na mwamko, ambacho kitaweza kuunganisha kati ya elimu ya kitaaluma na kushikamana na tunu, misingi na kanuni za maadili.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha